Na Mayasa Mariwata
MKURUGENZI wa RJ Company, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameshindwa kumzika baba mdogo wa mkurugenzi mwenza wa kampuni hiyo, Blandina Chagula, Clement Kiyenze Chagula.
Mzee huyo alifariki katika Hospitali ya Muhimbili kutokana na
matatizo ya presha na figo yaliyokuwa yakimsumbua na kuzikwa katika
Makaburi ya Kinondoni jijini Dar ambapo wasanii mbalimbali wa filamu
nchini walishiriki akiwemo Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete.MKURUGENZI wa RJ Company, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameshindwa kumzika baba mdogo wa mkurugenzi mwenza wa kampuni hiyo, Blandina Chagula, Clement Kiyenze Chagula.
Alipoulizwa Ray kwa nini hakuhudhuria mazishi hayo, alisema:
“Ukweli ni kwamba mimi sipo Dar. Ndiyo maana sijaonekana huko kwenye mazishi, nipo Mwanza katika shughuli zangu za kikazi, tuko pamoja lakini,” alisema Ray.