Stori: Hamida Hassan
Katika kuonyesha amechoshwa na upweke, mwanamitindo Jokate Mwegelo
‘Kidoti’ ameibuka na kusema kuwa sasa anasaka mwanaume wa kumuoa huku
akitaja vigezo vya anayestahili kumuita mume.
Jokate amekuwa msiri sana katika maisha
yake ya kimapenzi kiasi cha wengi kuamini ni msichana anayejiheshimu
sana ila aliwahi kuwa na uhusiano na mchezaji wa mpira wa kikapu,
Hasheem Thabeet anayekipiga kwenye Timu ya Oklahoma City Thunder ya
nchini Marekani.