Stori: Gladness Mallya
MTIFUANO mzito umeibuka kati ya mastaa wa Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na Baby Madaha baada ya kurushiana vijembe.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Shilole alisema anamshangaa Madaha kwa kukosa hofu ya Mungu, huku akimchana kuwa, haweki akiba, anaishi maisha ya kutegemea shoo ndiyo maana anaulalamikia mwezi huu.
Madaha alivyoelezwa kuhusu maoni ya Shilole, alikuja juu na kutema cheche: “Shilole anatafuta kiki kupitia jina langu, kwanza si hadhi yangu. Siwezi kujibishana na msanii anayetegemea shoo za kwenye vigodoro, akatafute pa kutokea.”