MISS Tanzania 2006/07 Wema Sepetu amesema ugonjwa wa
ngozi ulioshambulia sehemu ya shavu lake la kushoto umeharibu urembo
wake na kumfanya ashindwe kutoka.
MISS Tanzania 2006/07 Wema Sepetu amesema ugonjwa wa ngozi ulioshambulia sehemu ya shavu lake la kushoto umeharibu urembo wake na kumfanya ashindwe kutoka.
Akizungumza kwa huzuni, Wema alisema hakutegemea kama tatizo hilo
lingekuwa kubwa, kwani lilianza kama kipele kidogo ambacho baadaye
sehemu kubwa ilivimba na kuharibu mwonekano wake.
“Ulianza muwasho, kikawa kipele kisha kikageuka kama kishilingi.
Nilipokwenda hospitali nilipewa dawa ya crime ya kupaka, mimi
nikachua eneo lililoathirika, kumbe ndiyo nikawa nasababisha matatizo,
kukavimba zaidi kama unavyoona,” alisema Wema ambaye alikataa kupigwa
picha.