Mwaka
 2012, Tamasha la Usiku wa Matumaini (Night of Hope), lilikuwa kubwa 
sana, 2013 likatisha zaidi kutokana na muundo mzima wa burudani, 
jumlisha na historia iliyoandikwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa 
Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
Staa wa Bongo Movie,Irine Uwoya
Dk. Kikwete alikuwa mgeni rasmi, alizungumza na umati mkubwa 
uliohudhuria lakini hakuishia hapo, aliandika historia pale alipokagua 
wachezaji wa timu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Simba na 
Yanga, akasimama katikati ya uwanja na kupuliza kipyenga kuashiria 
kuanza kwa mchezo.Haikuwahi kutokea kabla! Kile alichokifanya Rais Jakaya Kikwete kilithibitisha ubora wa Tamasha la Usiku wa Matumaini. Mahudhurio ya watazamaji na kila kilichochukua nafasi, kilisherehesha dhana kwamba Night of Hope ni tamasha kubwa kuliko lolote lile ndani ya nchi.
Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee, alipanda ulingoni na kuchapana masumbwi na staa wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper, msisimko mwingine ukawa kati ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Mara, Ester Bulaya ‘aliyebatuana’ na nyota mwingine wa filamu, Aunt Ezekiel.
Nani aliamini haya yangetokea? Mastaa 
wakubwa wa muziki Afrika Mashariki, Dk. Jose Chameleone, CMB Prezzo, 
Diamond Platinum, TMK Wanaume Halisi, Wanaume Family, Chid Benz, H-Baba 
na wengine wengi  wameshabadilishana kipaza sauti ndani ya Uwanja wa 
Taifa, Dar es Salaam kwa miaka miwili mfululizo.
Bendi za FM Academia, Msondo Ngoma na Sikinde, zimeshafanya makubwa katika upande wa muziki wa dansi, Mzee Yusuf ‘Mfalme’ na Kundi la Jahazi Modern Taarab pamoja na Khadija Kopa ‘Malkia’ akiwa na timu yake ya Tot Taarab, wameshafanya mambo mazito katika tamasha hilo misimu iliyopita.
Jose Chamelione.
Isisahaulike mechi ya soka baina ya mastaa wa Bongo Movie na Bongo 
Flava, huku upande wa muziki wa Injili, waimbaji wakubwa kutoka ndani na
 nje ya nchi, wakifikisha neno la kumtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji.Bendi za FM Academia, Msondo Ngoma na Sikinde, zimeshafanya makubwa katika upande wa muziki wa dansi, Mzee Yusuf ‘Mfalme’ na Kundi la Jahazi Modern Taarab pamoja na Khadija Kopa ‘Malkia’ akiwa na timu yake ya Tot Taarab, wameshafanya mambo mazito katika tamasha hilo misimu iliyopita.
HESHIMA YA MWAKA 2014
Tamasha la Usiku wa Matumaini mwaka 2014, linatarajiwa kufanyika Agosti 8, yaani Nanenane ambayo ni Sikukuu ya Kitaifa ya Wakulima, tofauti na miaka iliyopita ambapo Night of Hope ilifanyika Julai 7, yaani Sabasaba ambayo ni Sikukuu ya Kitaifa ya Maonesho ya Biashara.
Mabadiliko haya yametokana na ukweli kwamba Sabasaba ya mwaka huu, imeingiliana na mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, kwa hiyo kamati ya maandalizi ya Night of Hope iliketi na kuamua tamasha hilo lifanyike Nanenane, kwa heshima ya waumini wa Dini ya Kiislamu.
Mwaka huu, tamasha limeboreshwa sana kwa upande wa burudani. Msanii anayechanua vizuri kutoka Nigeria, Yemi Alade, anayetamba na wimbo wake Johnny, atakutana na Watanzania na kufanya shoo ya kiwango cha juu.
Ipo mechi ya wabunge, Simba dhidi ya Yanga, wasanii wa Bongo Flava kuchuana na Bongo Movie. Mastaa wa filamu, Irene Uwoya na Jacqueline Wolper watachapana makonde. Supastaa Wema Sepetu atawapa raha Wabongo kwa kuimba nyimbo za boy friend wake Diamond pamoja na burudani nyingine kibao. Hakuna tamasha kama Usiku wa Matumaini.





