Wanawake
watatu katika soko la mkulima Tabora mjini wamejikuta wakipeana kipigo
kikali mchana kweupe wakati walipokuwa wakifanya biashara za mboga mboga
hatua ambayo ilisababisha kuharibu sehemu ya bidhaa wanazouza.
Chanzo cha ugomvi huo kimetokana na mmoja wa wanawake hao kuwa mbabe kwa wenzake na hivyo kushindwa kumvumilia kutokana na vituko vyake. |
muda mfupi baadaye waliamuliwa ugomvi huo na askari polisi Fakih Abdul aliyekuwa akipita sokoni hapo.