Na Gladness Mallya
MTABIRI maarufu nchini, Hassan Yahya Hussein amelitabiria penzi la waigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ na Chuchu Hans kuwa litakuwa na mafanikio makubwa kwani wanaendana.
MTABIRI maarufu nchini, Hassan Yahya Hussein amelitabiria penzi la waigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ na Chuchu Hans kuwa litakuwa na mafanikio makubwa kwani wanaendana.
Akizungumza na Amani, Hussein alisema kinyota Ray nyota yake ni aina ya Mashuke ambapo Chuchu nyota yake ni Mapacha ambazo zinaendana kwani wanashirikiana sayari moja ambayo ni Mercury na siku yao ya bahati ni Jumatano.
“Japokuwa Ray amehangaika sana lakini kwa Chuchu amefika hivyo ajitahidi kutulia na asihangaike tena na wanawake kwani huyu wanaendana tofauti na wale wanaotajwa kuwa alikuwa na uhusiano nao yaani Johari na Mainda,” alisema Hussein.