Waumini wapatao 29 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni jana jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kufanya fujo hadharani katika Kanisa la Moravian lililopo Mwananyamala-Msisiri ” A” Wilaya ya Kionondoni.
Katika kesi hiyo iliyounguruma kwa muda wa saa mbilli imeelezwa kuwa
Julai 20 mwaka huu katika kanisa hilo lililopo eneo la Mwananyamala
Msisiri ‘A’ waumini hao kwa pamoja walifanya fujo zilizosababisha
kuhatarisha amani.
Kesi hiyo iliyosomwa na mwendesha mashitaka wa serikali, Credo Rugajo
mbele hakimu mwandamizi wa mahakama hiyo Boniphace Lihamwike,
ilidaiwa kuwa Julai 20 waumini walianzisha mzozo uliosababisha waumini
kupigana na kusababaisha askari polisi kutumia nguvu kubwa
kutuliza fujo hizo ikiwa ni pamoja na kutumia mabomu ya machozi.
Baada ya kusikiliza kesi pande zote mbili, Hakimu Lihamwike alisema
dhamana iko wazi kwa kila mtuhumiwa kuwa na mdhamini mmoja
anayeaminika na shilingi milioni moja kimaandishi kwa kila mmoja.