MWANAMKE mmoja
aliyejulikana kwa jina la Fatuma Said mkazi wa Kitunda, Ilala jijini
Dar es Salaam anashikiliwa na Polisi baada ya kummwagia maji ya moto
mumewe sehemu za siri na tumboni kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa
kimapenzi, tukio lililotokea Julai 16 mwaka huu, huko Kitunda.
Majeruhi Adam Rashid akiwa amelazwa katika Hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam kwa majeraha ya maji ya moto.
Chanzo chetu cha habari kililiambia
paparazi kuwa tukio hilo lilitokea saa 12.30 jioni baada ya mwanaume
huyo, Adam Rashid ambaye ana wake wawili, kwenda katika nyumba anayoishi
mke mkubwa akiwa ameandamana na mke mdogo, kwa lengo la kupata maji ya
kuoga na kubadili nguo, akitokea kituo kidogo cha Polisi Stakishari,
ambako aliwekewa dhamana kwa shauri lililokuwa likimkabili.
Inadaiwa kuwa baada ya kuwekewa dhamana
hiyo, Adam na mkewe mdogo, Aisha Juma, waliamua kwenda nyumba anayoishi
mke mkubwa, ambayo inamilikiwa na mwanaume huyo, kwa ajili ya kuoga na
kubadili nguo, wakiamini kuwa kusingekuwa na matatizo yoyote kwa vile
wanawake wote wawili anaishi nao kihalali na wanafahamiana.
Inasemekana kuwa baada ya kufika
nyumbani hapo, Adam alimtaka mwanaye kumwandalia maji ya kuoga na
akimaliza apewe bukta, ili aweze kuondoka na mke mdogo kuelekea
wanakoishi, lakini wakati hayo yakifanyika, bi mkubwa alianza kutoa
maneno machafu ya kejeli, yaliyoonyesha wazi kuwa alikuwa na wivu wa
kimapenzi.
Majeraha ya maji ya moto aliyopata Bw. Adam Rashid.
Baada ya mwanaume huyo kumaliza kuoga na
kutoka nje, inadaiwa mkewe mkubwa alijitokeza akiwa amebeba sufuria
iliyokuwa na maji ya moto, yanayodaiwa kuwa yalitakiwa kutumika kwa
ajili ya kupikia wali na kumwagia tumboni na sehemu za siri, huku
akiendelea kumtolea maneno ya kashfa.
MAJERUHI ALONGA
Akiwa amelazwa katika wodi namba tatu kwenye hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam, majeruhi Adamu Rashid alisema Julai 16 mwaka huu alienda nyumbani kwake akiwa ameandamana na mke wake mdogo, lakini akashangazwa na kitendo cha bi mkubwa kuanza kubwata na kumwuliza alichokifuata, kana kwamba amesahau kama pale ni kwake na wote ni wake zake.
Akiwa amelazwa katika wodi namba tatu kwenye hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam, majeruhi Adamu Rashid alisema Julai 16 mwaka huu alienda nyumbani kwake akiwa ameandamana na mke wake mdogo, lakini akashangazwa na kitendo cha bi mkubwa kuanza kubwata na kumwuliza alichokifuata, kana kwamba amesahau kama pale ni kwake na wote ni wake zake.
“Baada ya kunimwagia maji, mke wangu
mdogo alilia sana kwa uchungu, majirani wakanichukua na kunipeleka
Polisi ambako tulimkuta bi mkubwa akiwa anaandikisha maelezo kuwa mimi
nimempiga, kuona vile askari walimgeuzia kibao na kumwingiza ndani kwa
ajili ya mahojiano zaidi.”
MKE MDOGO NAE
“Ndugu mwandishi, mimi na mume wangu tulienda hadi kwa mke mkubwa bila wasiwasi maana na mimi pale ni kwangu kwa sababu nyumba ya mume wangu halali, lakini tulipofika tuliambulia maneno machafu na kejeli.
“Ndugu mwandishi, mimi na mume wangu tulienda hadi kwa mke mkubwa bila wasiwasi maana na mimi pale ni kwangu kwa sababu nyumba ya mume wangu halali, lakini tulipofika tuliambulia maneno machafu na kejeli.
Mke mkubwa alihoji kwa jeuri kitu gani
tulichokifuata pale, mume wangu alikuwa akimjibu kuwa hapa nipo kwangu
na huyu niliyekuja naye ni mke wangu halali, mbona unanifanyia mambo
ambayo siyaelewi, yule hakuelewa, aliendelea tu na maneno yake
machafu.”
KAMANDA WA POLISI
Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Ilala, SACP
Marieth Minagi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
na kusema mtuhumiwa huyo anashililiwa katika
kituo cha polisi Wilaya ya kipolisi Ukonga na
amefunguliwa jalada na kupewa namba
RB/STK/9438/2014 KUJERUHI
na uchunguzi unaendelea.....