Featured Posts

Wednesday, July 23, 2014

UNAAMBIWA KANISA LA MORAVIAN NI FULL SINEMA...WAUMINI WACHEZESHEANA VICHAPO VYA HAJA

ILIKUWA ni full sinema mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya waumini wa Kanisa la Moravian, lililopo Mwananyamala Msisiri jijini Dar es Salaam kuanzisha vurugu kubwa zilizozimwa na Jeshi la Polisi baada ya kulazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi ili kuwadhibiti na hatimaye kuwakamata 29 kati yao.


Waumini wakipandishwa kwenye difenda.
Inadaiwa kuwa waumini wa kanisa hilo lenye jengo la ghorofa moja walikuwa katika mgogoro uliotokana na madai ya ubadhilifu wa fedha, hivyo kuwafanya kugawana sehemu za kufanyia ibada, kundi moja likisali chini na jingine juu, kila moja likiwa na mchungaji wake, ambao ndiyo waliokuwa wakiongoza mzozo huo.
Ghafla, kundi lililokuwa likisali chini likaamua kuwafungia milango wale wa juu na kuwafanya kuendesha ibada yao nje, chini ya mwembe kwa siku kadhaa kabla ya kuamua kuvamia kanisani ili nao wasali kama wenzao, ambao walikataliwa na hivyo timbwili kubwa kuanza.
Askari wakiwa na silaha.
Wakiwa na fimbo na mawe, waumini hao wa makundi yote mawili walileta tafrani kubwa kabla ya wasamaria wema kutoa taarifa Polisi ambao walifika eneo la tukio na kujaribu kutuliza ghasia lakini bila mafanikio, hadi walipoamua kutumia mabomu ya kutoa machozi na kufanikiwa kudhibiti vurugu hizo zilizosababisha mtu mmoja kujeruhiwa, sambamba na kuwakamata waumini 29 ambao walishikiliwa katika kituo cha polisi Oyesterbay jijini Dar es Salaam.
Waumini chini ya ulinzi.
Habari ambazo hazikuweza kuthibitishwa mara moja zinasema chanzo cha mgogoro huo ni ubadhilifu wa fedha za kanisa, baada ya kugundulika kuwa nyumba moja iliyonunuliwa, ilipewa thamani kubwa ya pesa ambazo zilishatolewa, lakini mwenye nyumba alikataa kutoa hati akitaka kumaliziwa fedha zake, jambo lililowashangaza waumini ambao walihoji.
Bango la kanisa hilo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba hatua za kisheria zitafuata baada ya uchunguzi kukamilika.

TUMEAMIA HUKU