MWENYEKITI wa Klabu ya Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amefungukia madai ya kumtenga msanii mwenzao, Coletha Raymond ‘Koleta’ kipindi alipokuwa anaumwa.
Awali, madai yalipenyezwa kuwa, klabu hiyo ilimtenga Koleta kipindi alipokuwa akiumwa ambapo alilazwa katika Hospitali ya Kairuki kwa kilichodaiwa hakuwa na ushirikiano kati yake na wasanii wenzie.
Akikanusha taarifa hizo pamoja na kutomchangia fedha, Steve alisema:
Akikanusha taarifa hizo pamoja na kutomchangia fedha, Steve alisema:
“Tukianza kusema kila anayeumwa tuwe tunamchangia wanachama watakimbia na mfuko tuliokuwa nao utaisha na tutashindwa kufikia malengo, lakini sikupata taarifa za ugonjwa kuhusu Koleta na hata ningezipata asingeachwa,” alisema Steve huku Koleta akisisitiza kuwa anatengwa.
“Sijui kuna nini kinaendelea kwa upande wangu na sifahamu kwa nini sipewi taarifa kwa wakati na uongozi wangu kama ilivyo kwa wasanii wengine wa Bongo Movie, najisikia vibaya sana,” alisema Koleta.