Na Gladness Mallya
KUTOKANA na hivi karibuni mumewe, Hamis Baba ‘H. Baba’ kuugua ugonjwa wa homa ya Dengue ‘Dengi’ na kulazwa Muhimbili, msanii wa filamu Bongo, Flora Mvungi amesema alijikuta kwenye wakati mgumu kuhofia mumewe angepoteza maisha.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Flora alisema ni Mungu tu mumewe kupona kwani alikuwa katika hali mbaya ambayo mpaka yeye kama mkewe alikuwa na hofu kubwa ya kifo haswa ukizingatia vifo vya wasanii vilivyotokea mfululizo.
“Nilipoona wasanii wenzangu wakifariki dunia na mume wangu kuzidiwa mpaka kulazwa Muhimbili, nilikuwa nina hofu kubwa ya kifo lakini namshukuru Mungu amepona na tunaendelea na maisha kama kawaida, dengue noma sana,” alisema Flora.