Mtangazaji wa Kipindi cha The One Show, Jokate Mwegelo ‘Jojo’ amefunguka kuwa hahusiki na kuvunjika kwa ndoa ya Khadija Shaibu ‘Dida’ kwani ni mshikaji wake na wanaheshimiana.
Akijibu tuhuma kuwa, yeye anahusika na kuparaganyika kwa ndoa hiyo kufuatia ‘ku-fall in love’ kwa mume wa Dida, Edzen Jumanne ambaye ni mtangazaji mwenzake, Jokate alisema:
“Yaani watu wanapenda kuungaunga maneno kweli, jamani mimi siwezi hata siku moja kuwa na Edzen, ni mfanyakazi mwenzangu halafu Dida ni mshikaji wangu siwezi kabisa, tena wasitake kunitibulia.”