Msanii wa maigizo na muziki wa kizazi cha leo, Zena Mohammed 'Shilole' amekuja juu na kusema anashangazwa na habari zilizozagaa mjini kuwa yeye amekataliwa ukweni....
Akiongea na Mpekuzi, Shilole amesema: "Nashangaa watu wanasema eti nimekataliwa ukweni kisa umri wangu kuwa mkubwa kuliko wa mwanaume. Ninachokijua mimi umri haujalishi katika mapenzi, kikubwa ni upendo wa kweli na kuheshimiana.
"Habari za mimi kukataliwa ukweni hazina ukweli wowote, na wala hakuna mtu niliyezungumza naye kuhusiana na hilo swala na wala hakuna ndugu yeyote wa Nuh Mziwanda aliyeonysha kutonipenda.
"Nilipokelewa kwa furaha sana Ukweni na habari njema ni kwamba hivi karibuni mtarajie kuona ndoa ili wanafiki tuwafunge midomo yao," alisema Shilole