MSANII wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ (19) amewataka watu wanaomsema vibaya kuhusu kuwa na uhusiano wa kimapenzi wamuache kwani anaonesha urijali wake.
“Mimi nawashangaa sana watu wanaonisema kwa sababu eti nina demu, nimeamua kuonyesha urijali wangu au wanataka nigeuke shoga mbona wasanii kibao ambao ninalingana nao wana wanawake?” alihoji Dogo Janja ambaye sasa amerejea katika Kundi la Tip Top Connection alilokuwa amelikacha kwa muda.