Kulia ni Jacob Mayani kinara wa ubakaji,ulawiti na kutoboa macho watoto Shinyanga
Mtuhumiwa aliyekuwa akikabiliwa na kesi za ubakaji na kulawiti watoto katika Manispaa ya Shinyanga amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kesi tatu tofauti.
Mtuhumiwa
huyo Jacob Mayani au maarufu kwa jina la Boy mwenye umri wa miaka 28
mkazi wa manspaa ya Shinyanga amehukumiwa vifungo vitatu vya maisha
kwenye MAHAKAMA ya Hakimu mkazi Mfawidhi Shinyanga.
Jacob
Mayani ambaye alituhumiwa kuhusika na matukio tofauti ya ubakaji na
kulawiti watoto chini ya miaka 10 sanjari na kuwatoboa macho amejikuta
akiishia gerezani.