MASTAA ‘tega nikutege’ katika Kiwanda cha Filamu Bongo, Miriam Jolwa
‘Jini Kabula’ na shostito wake, Jacqueline Pentzel ‘Jack wa Chuz’
wamebambwa wakinyonyana ndimi, Amani lina ushahidi mkononi.
Wawili
hao walinaswa hivi karibuni maeneo ya Mango Garden, Kinondoni, Dar es
salaam karibu na ofisi za ‘Jumba la Dhahabu’ wakiwa katika hali ya
kimahaba huku wakijua kuwa, kitendo hicho hakiendani na utamaduni wa
Mtanzania.
Katika pozi lao hilo, Kabula alionesha kumganda zaidi
Jack huku mkono wake mmoja akiupeleka kwenye kiuno na vidole vya mkono
wa pili vikiwa masikioni mwa mwenzake huyo.
“Khaa!
Jamani mbona unapiga picha bila idhini yetu? Futa bwana, sisi tuko
kwenye starehe zetu na ole wako tuzione gazetini,” aliropoka Jack baada
ya kuona mwanga wa kamera ukiwamulika na kubaini kwamba, wamepigwa
picha.
Wakati akija juu, hali ilikuwa tofauti kwa upande wa ‘mpenziwe’ Jini Kabula ambapo yeye alionekana kukifurahia kitendo hicho.
Mwandishi wetu hakuacha ‘gepu’ kukamilisha habari hii, alimfuata na kumuuliza kulikoni afanye kitendo hicho cha aibu:
“Wewe
si umeshapiga picha, basi chukua ‘taimu’ yako, tuache na mambo yetu.
Mimi naona ni kawaida kwani sisi hatuna hisia? Kama tumechoka na wanaume
je!” Alikoroma Jini Kabula huku akimtazama mwandishi kuanzia chini hadi
juu kama ishara ya kumdharau.
Baadhi ya watu waliokuwa katika
eneo hilo na kushuhudia, walisikika wakilaani kitendo hicho huku
wakisema kuwa ni uchafu mtupu. Walisema wasanii hao wamekithiri kwa
vitendo viovu.
“Afadhali umewakuta ‘laivu’ maana huu ni uchafu.
Tena hawa wamezoea, maana kila wakifanya maovu wanakanusha, tumewachoka.
Na kama kioo cha jamii ndiyo hivi, hakuna maana,” alisema mwanamke
mmoja mwenye umri kati ya miaka 45 hadi 50.
Baadhi ya wasanii wa ‘Jumba la Dhahabu’, walitoka nje na kukuta watu wamejazana wakiwashangaa wasanii wenzao kwa kitendo hicho.
Jack
wa Chuz na Jini Kabula ni wasanii ambao hawakauki skendo chafu
zinazomomonyoa maadili ya kitanzania zikiwemo za kuchangia wanaume na
kuvaa nguo fupi za aibu kinyume kabisa na ‘taito’ yao.
Milioni 392 Zajenga Barabara HEWA Dar es Salaam
-
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob amebaini matumizi ya Sh392
milioni zilizoandikwa kwenye taarifa ya manispaa hiyo kuwa zimetumika kwa
ajili y...