Uongozi
wa Yanga umesema Mwenyekiti wa Kamati ya ujezi wa jengo la Mafia,
Ridhiwani Kikwete siyo mwanachama wa klabu hiyo kwa kuwa hajalipa ada
yake kwa miezi sita mfululizo.
Katika
taarifa yake iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na kusainiwa na
Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto ilieleza kitendo cha Ridhiwani kupinga
hatua ya Wajumbe wa Bodi ya Udhamini na wanachama wa Yanga kwa pamoja
kumuongezea muda wa mwaka mmoja, mwenyekiti wao, Yusuf Manji hayana
uzito kwa kuwa siyo mwanachama.
“Ridhwani
Kikwete hajalipa ada zake za uanachama kwa miezi zaidi ya 6 mfululizo
na kwa mujibu wa Katiba ya Yanga ibara ya 13 kipengele cha pili ambacho
kinasema kuwa endapo mwanachama hajalipa ada yake kwa muda wa zaidi ya
miezi sita mfululizo atakuwa amekoma kuwa mwanachama wa Yanga.”
“Maoni
aliyoyatoa hayana uzito wa mwanachama wa Yanga, labda alikuwa akitimiza
haki yake ya kutoa maoni kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, tunaamini kama angekuwa ni Mwanachama hai wa Yanga angetoa
maoni yake kwenye Mkutano wa dharura wa Wanachama uliofanyika Juni
Mosi. Pia angeweza kutoa kwenye kitabu cha maoni ya kupinga maazimio ya
Mkutano huo kilichowekwa hapa klabuni kuanzia Juni 23 hadi 27, hakuna
aliyesaini zaidi ya mwenyekiti, Manji.

Ridhiwani Kikwete
“Niwakumbushe
wanachama wa Yanga sehemu ya kuchangia maoni yao ni kwenye vikao vya
Wanachama na siyo kwenye vyombo vya habari, wasitafute umaarufu kwa
njia za kubomoa kuliko kujenga wala wasiwadhalilishe waliojitosa kwa
hali na mali kuisaidia Yanga kuwa bora kama Mama Fatma Karume wenye
historia ndefu Yanga, tunaona ni sawa na udhalilishaji kwake, kwa kweli
inasikitisha sana.Taarifa
hiyo ya Yanga imekuja ikiwa ni siku moja baadaya Ridhiwani kukaririwa
na gazeti hili akisema haridhishwi na mambo ya migogoro ya kikatiba
yanayoendelea ndani ya Yanga.