Pichani juu ni Kishoka wa Tanesco aliyekamatwa Mlimani City.
TAPELI lililokubuhu
kwa masuala ya kulaghai watu kwa njia ya kujifanya kishoka washirika la
Umeme Nchini, Tanesco, jana asubuhi limedakwa baada ya kuwekewa mtego
walipokuwa wakitaka kutapeli kwa mmoja wa Afisa wa Habari wa Kituo cha
Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma- Ledama.
Kwa
mujibu wa Bi. Usia akieleza tukio hilo, alidai kuwa tapeli huyo alifika
asubuhi akiwa na wenzake sita, nyumbani kwake wakasema wanatoka Tanesco
wamekuja kucheki mita ya Luku. Hata hivyo wakakorokocha wakasema mita
imechezewa kwa hiyo wanakata Umeme na kung'oa mita, eti waliona kwenye
GPS yao kuwa Umeme hauendi vema.
“wakasema
fidia na kurudisha umeme kiofisi ni milioni 8! ila tukiwapa milioni 2
wataturudishia. nikawauliza kama mita imechezewa mbona tunanunua umemewa
laki 3 kwamwezi? si ingepaswa tulipe kidogo? wakasema wakati mwingine
wakiweka hiyo resistance (eti ndo kifaa cha kuiba Umeme) huwa
kinafyatuka halafu Umeme unakwenda zaidi! “ alielezea Bi. Usia.
Na
kuongeza kuwa vishoka hao wakakata Umeme wakaondoka, tujipange.
tujadiliana na mzee tukapata mashaka maana walikuwa wakali halafu
wanalazimisha mambo, wamevaa vitambulisho lakini wamevigeuza kwahiyo
havisomeki. tukapiga simu Tanesco kuwauliza wakasema hao ni vishoka
tuitePolisi, basi tukawapigia simu waje wachukue laki tano waturudishie
Umeme, mengine Jumatatu. wakaja fasta wakarudisha Umeme, nikawaambia
naenda aTM wasubiri nikawaacha na mzee nikatoka mbio mpaka Polisi chuo
nikawahadithia wakanipa Polisi 3 nikaja nao nyumbani, tukawakuta
wameondoka.
Mzee
akawapigia simu waje hela imepatikana wakasema tukutane Mlimani City,
tukafanikiwa kukamata mmoja wengine wakakimbia. tumemuacha selo,
tukaandikisha maelezo. tunasubiri hatua itakayofuata.