Hapa ni
katika eneo la dharura katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga ambapo
majeruhi 29 hadi sasa wamepokelewa kufuatia ajali ya gari aina ya fuso
iliyokuwa imebeba watu wengi pamoja na mizigo kuelekea katika mnada wa
Mhunze uliopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.Ajali hiyo imetokea
asubuhi ya leo Alhamis.Pichani majeruhi waliendelea kuhudumiwa na
wataalam wa afya katika hospotali ya mkoa wa Shinyanga
Kwa mujibu wa kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Maguja Daniel ameiambia malunde1 blog kuwa mpaka sasa wamepokea miili miwili ya marehemu na majeruhi 29 |
Huduma inaendelea kutolewa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga
|
Baadhi
ya majeruhi wameiambia blog Hii kuwa gari aina ya fuso waliyokuwa
wamepanda tena kwa kujazana ilikuwa inafukuzana na fuso nyingine na
ghafla walijikuta wakiwa wameshapinduka
Kulia
ni kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Maguja
Daniel akichukua maelezo kutoka kwa askari wa usalama barabarani
|
Kaimu
mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Maguja Daniel
akizungumza na waandishi wa habari hivi punde-Picha zote na Kadama
Malunde-Malunde1 blog