Featured Posts

Thursday, July 24, 2014

TAZAMA BALAA LA HAWA BONGO MOVIE WAALIVYOAMUA KUKAA UTUPU COCO BEACH


BAADHI ya wasanii wa filamu za Kibongo hivi karibuni walinaswa wakifanya vitendo vichafu katika eneo lao la kurekodia ‘location’ pande za Oysterbay jijini Dar, Ijumaa lina uthibitisho wa kutosha.
Wasanii wa filamu wakipozi kwa picha tata.
Kwa mujibu wa chanzo chetu wasanii hao walinaswa wakifanya vitendo hivyo vilivyo nje ya maadili ya Mtanzania kwa uwazi bila ya kumuogopa mtu yeyote.
Chanzo chetu kilijipenyeza katika kambi ya wasanii hao iliyopo eneo hilo na kuwanasa wakifanya vitendo hivyo vichafu.
…Pozi lingine la kichokozi la wasanii hao waliokuwa lokesheni.
“Wameweka kambi kwenye nyumba moja Mikocheni na wamekuwa wakienda kushuti kwenye Ufukwe wa Coco, yaani nimekuwa nikiwafuatilia matendo yao, siyo mazuri. Wanavaa nguo nusu utupu, wanafanya vitendo vinavyoashiria usagaji mbele za watu bila aibu, njooni muwafichue.
“Kuna picha ambazo nimewapiga bila wao kujijua, zinatia kinyaa, mbaya zaidi wengi wao ni wadogowadogo na huenda wamewadanganya wazazi wao kuwa wameenda shule kumbe wapo huku,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya paparazi wetu kushibishwa madai hayo na kuziona picha hizo chafu,  aliwafuatilia wasanii hao na kuwatambua kwa majina  waliohusika kufanya uchafu huo kuwa ni Leticia, Ania pamoja na  mchekeshaji wa siku nyingi, Jabir Ally ‘Wajajo’.

Alipotafutwa Wajajo kuzungumzia picha hizo alisema: “Sidhani kama ni makosa watu kujiachia ufukweni, labda kwa waliofanya vitendo vya kisagaji ndiyo watakuwa wamekosea…tulikuwa lokesheni tukirekodi filamu tukawa tumejiachia, inawezekana wengine walipitiliza.

TUMEAMIA HUKU