STAAwa sinema za Kibongo, Lucy Komba, amedaiwa kutengwa na wasanii wenzake wa Klabu ya Bongo Movie kwa kosa la kuwatolea lugha za kejeli.Staa wa sinema za Kibongo, Lucy Komba,
Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa, Bongo Movie wamemsusia msanii huyo katika vikao vya harusi yake kwa madai kuwa aliwahi kuwaponda kwenye vyombo vya habari kuwa klabu hiyo si chochote kwake.
Alipotafutwa na paparazi wetu, Lucy ambaye anatarajia kufunga pingu za maisha Septemba, mwaka huu, alisema hakumbuki kama aliwahi kuwakejeli wasanii hao isipokuwa wengi wamekuwa wakimjadili kwa suala hilo na sasa hawahudhurii kwenye vikao vya harusi yake.
“Mimi hata sikumbuki kama niliwahi kuongea hayo kwenye vyombo vya habari na kama niliongea labda walinielewa tofauti na kauli niliyoitoa, sioni sababu ya kuwekeana bifu ila kwa anayetaka acha aendelee,” alisema Lucy.