Featured Posts

Monday, July 14, 2014

MASKINI PENZI LA SHILOLE NA NUHU MZIWANDA LAINGIA KASORO NZITO, SOMA HAPA UHABARIKE ZAIDI

Habari zinadai kwamba baadhi ya ndugu wa msanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda ambao ni wakwe wa staa wa muziki na filamu za Kibongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ hawamtaki kwa madai kuwa ana umri mkubwa kuliko ndugu yao. 
Staa wa muziki na filamu za Kibongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’
 Wakizungumza na Ijumaa Wikienda kwa nyakati tofauti, baadhi ya wanandugu hao (majina yanahifadhiwa) walisema umri wa Shilole siyo wa kuishi na ndugu yao, Mziwanda kwani hawaendani.
“Ukweli ni kwamba mapenzi hayaingiliwi lakini tunaumia kuona ndugu yetu katika penzi zito na Shilole ambaye hawaendani kiumri,” alidai mmoja wa ndugu hao.


‘Shilole’ akiwa na mpenzi wake ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda
 Alipotafutwa Shilole ili kufikishiwa ujumbe wa ndugu hao kwamba hawamtaki, simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa.

TUMEAMIA HUKU