Featured Posts

Tuesday, September 2, 2014

AFISA USALAMA FEKI ANASWA NA.BUNDUKI KIBAO

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam linamshikilia mtu mmoja
anayefahamika kwa jina la Gunner Meena ( 40)
mkazi wa Kinyerezi, Segerea , Dar es Salaam,
kwa tuhuma za kujifanya mtumishi wa Idara
ya Usalama wa Taifa .
Tukio la mwisho lililomfanya akamatwe ni pale
alipomtishia mfanyabiashara mwenye asili ya
Kisomali aitwaye Abdi Dalmar, ili ampe Tshs
25, 000, 000 /= ama sivyo angechukua hatua
chini ya Sheria ya Usalama wa Taifa .
Aidha jeshi hilo katika kuendesha oparesheni
zake za kutokomeza ujambazi wa kutumia
silaha limefanikiwa kukamata bastola nne na
shot- gun moja wiki hii .

TUMEAMIA HUKU