Kifo cha Amina Ngaluma ‘Japanese’ kilitokea baada ya kuumwa kwa siku nne ambapo mume wake alipozungumza na millardayo.com amesema kiongozi wa band yao huko Thailand alimwambia Amina alilazwa hospitali kutokana na maumivu makali ya kichwa,mwili wa Amina Ngaluma ulipokelewa jana Mei 23 na saa 6 kasoro za usiku taratibu za kuutoa mwili huo nje zilikamilika.
Amina ngaluma amezikwa mchana wa leo kwenye makaburi ya Machimbo Mnarani Dar es salaam.mahali ambako inaishi familia yake.