Msanii Wa Muziki wa Bongofleva mwenye
jina kubwa Town na mwenye Mkwanja mkubwa hapa nchini Nasseeb Abdulmaliki
“Diamond” amejitokeza na kukanusha kuwa hahusiki na biashara ya madawa
ya kulevya. Amesema...
Ni kwa muda mrefu sasa kumekuwa na
taarifa za Diamond kujihusisha na biashara hiyo hasa kutokana na ukaribu
wake na wfanya biashara wakubwa wa dawa za kulevya wenye maskani yao
nchini Afrika Kusini. Taarifa zaidi zinasema ni wafanyabiashara hao
waliohusika kwa karibu kuusafirisha mwili wa marehemu Albert Mangwair,
aliyefia huko huko Afrika Kusini ambaye taarifa za kifo chake
ziligubikwa na matumizi ya madawa ya kulevya.
Akikanusha taarifa hizo Diamond alisema
“ni kweli mimi nina pesa za kutosha kuniwezesha kuishi maisha ninayotaka
lakini sijawahi kujihusisha na biashara hiyo. Kufanya kazi kwa bidii
kunalipa na kazi yangu inaonekana na ndiyo inayoniwezesha kuwa na fedha
ambazo leo watu wameanza kuzitilia shaka. Sielewi nia ya watu hawa ni
nini?”
Taarifa za Diamond kuhusishwa na mtandao
huu zimeanza kushika kasi kufuatia miongoni mwa watu wake wa karibu
kuonekana wakiwa karibu sana na akina Agnes Gerald “Masogange” (25) na
Melisa Edward (24) kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa Mwalimu JK
Nyerere wa Dar es Salaam kabla hawajapanda ndege kuelekea Afrika Kusini
ambako walikamatwa.
Milioni 392 Zajenga Barabara HEWA Dar es Salaam
-
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob amebaini matumizi ya Sh392
milioni zilizoandikwa kwenye taarifa ya manispaa hiyo kuwa zimetumika kwa
ajili y...