Featured Posts

Friday, July 18, 2014

DARASA LA WAKUBWA:FAHAMU JINSI SIMU INAVYOWEZA KUSAMBARATISHA MAHUSIANO YAKO.



Habari za masiku tele wadau wa blog hii, nawapenda sana maana pamoja na kuwa bila post mpya kwa muda mrefu bado mpo na mnaendelea kuwepo humu. Asanteni sana.
Leo napenda tujadiliane suala la simu za mikononi. Najua limeshazungumzwa sana mara nyingi katika vyombo mbali mbali, lakini leo mimi napenda kuingia ndani zaidi kwa kutoa tips on how you should handle ur 4ne ili mahusiano yako yadumu na yasivunjike kwa sababu tuu ya simu yako au ya mwenza wako.
Watu wengi sana wamekuwa wakijikuta katika wakati mgumu kwa sababu ya kitu hiki kidogo, simu!!! kwanini wewe unamiliki simu yako na ya mpenzi wako? kwanini humuamini? kwanini nawe pia hujiamini?  Je kama anakupenda kwa dhati anaweza kukucheat? kwa nini usimpe nafasi ajitambue kuliko kuwa mlinzi wa simu yake? Do u think ukijua anawasiliana na nani kutwa nzima ndo utakuwa na furaha maishani au utaongeza matatizo moyoni mwako na katika mahusiano yenu?

Maswali hayo machache tuu tujiulize kabla hatujaenda mbali. WHY?
Katika hali ya kawaida tuu hasa kibongobongo, ukikagua sana simu ya mweza wako utajikuta badala ya kupata furaha unapata stress ambazo hazina mpango!! Unaumiza moyo wako maana utajikuta unagundua vitu vingi vya ajabu na mahusiano yanaanza kuvurugika!

NINI CHA KUFANYA?
Uaminifu ni kitu kizuri, muonyeshe kuwa unamuamini sana. usimfuatilie kupita kiasi hasa katika simu yake ya mkononi. Mwache awe na uhuru na simu yake, muonyeshe kuwa bila yeye unaweza kuishi maana ukifuatilia sana simu yake, utaumia na ataprove kuwa bila yeye u ar nothing!! Unajua mtu ukimpa uhuru sana hata yeye anajishtukia na kushangaa inakuwaje, so hata kama anafanya ujinga atajirudi kwa kuona ni kiasi gani anakukosea na wakati wewe umetulia na unampenda.

Mpende kwa dhati, lakini haimaanishi ndo uwe mlinzi wa simu yake ya mkononi, utajiumiza bure na mapenzi wala hutoona raha yake. Tulia, anayekupenda utamjua tuu wala hana macho juu, hana mawasiliano yasiyokuwa na maana, anatulia na wewe.

TUMEAMIA HUKU