Davido ni mtu ambaye huwa anaonyesha
vitu vingi anavyonunua kama baadhi ya mastaa lakini kwa upande wa Davido
vinahusika vitu vya gharama sana. Ukicheki utaona post akionyesha saa
za Rolex ambazo zina material ya dhahabu, magari ya kifahari,nyumba na
vitu vingine.
Baada ya kuulizwa kuhusu ishu hii ya
kupenda kuonyesha mali zake kwenye instagram Davido alijibu,”Sitaweza
kuita kama ni kujionyesha kwa mali zangu. Yale ni magari yangu,zile pesa
zangu na pia ile ni page yangu.
Sio lazima uni follow kwenye instagram
wala kunifata kwenye mtandao wowote wa kijamii. Ingekuwa tofauti sana
kama nataka kujitangazia mali zangu basi ningetumia mabango ya
barabarani lakini sifanyi hivyo”