Featured Posts

Tuesday, September 23, 2014

MASKINI NORA AJUTA KUOLEWA MAPEMA, ADAI VIJANA SA HIVI WANAJIACHIA SANA

MAJUTO! Mwigizaji wa kitambo Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ amefunguka kuwa siku zote katika maisha yake anajuta kuolewa mapema kwani asingefanya hivyo angeweza kufanya mambo mengi na angekuwa mbali sana kisanii na kielimu. 

Mwigizaji wa kitambo Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ akipozi.
 Nora alisema kuwa kipindi alipoolewa na aliyekuwa mganga wa tiba za asili, marehemu
Ngwizikulu Jilala, alikuwa akimnyima uhuru wa kuendelea na sanaa na masomo.
 “Unajua kweli najuta sana mimi kuolewa mapema kama si hivyo ningeendeleza fani yangu na sasa ningekuwa mbali lakini kipindi chote cha ndoa nilisimama sikuweza tena kuigiza,” alisema Nora.
Msanii huyo amesema kwa sasa amerudi upya kwenye gemu na tayari ameandaa sinema mpya inayokwenda kwa jina la Msimamo Wangu ambayo imeshakamilika, itatoka hivi karibuni.

TUMEAMIA HUKU