Featured Posts

Tuesday, July 22, 2014

TAARIFA RASMI YA MTOTO ALIYENYONGWA NA KUTUPWA KISIMANI WILAYANI KAHAMA

Mtoto wa kike anayekadiriwa kuwa na wiki tatu amekutwa amefariki dunia baada ya kunyongwa na kutupwa na mama yake katika kisima kilichopo mtaa wa Nyasubi wilayani Kahama katika Mkoa wa Shinyanga.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga Justus Kamugisha amesema tukio hilo limetokea jana asubuhi mjini kahama.

Kamanda Kamugisha amesema mama wa mtoto huyo Rhoda Idedemya (18) mkazi wa Nyasubi ametenda tukio hilo na kujaribu kutoroka kabla ya kukamatwa na jeshi la polisi akiwa ndani ya gari la abiria liendalo Runzewe.
Mama wa mtoto huyo Rhoda Idedemya akiwa katika kituo cha polisi Kahama baada ya kukamatwa.
Mama mlezi wa mtuhumiwa aliyejitambulisha kwa jina la Christina au mama paulo amesema ameishi na mtuhumiwa huyo toka akiwa na ujauzito baada ya kumuomba hifadhi mpaka alipojifungua wiki tatu zilizopita.

Amesema Rhoda amekuwa na tabia ya kuondoka nyumbani na kumuacha mtoto zaidi ya masaa matano,na baada ya kukemewa alikiri kutorudia.

Christina amesema, hii leo akiwa kazini kwake,Rhoda alimfuata na kumuaga kuwa anakwenda Runzewe kwa kaka yake, na kwamba mtoto amempeleka kwa baba yake anayeishi mhungula hali iliyompa wasiwasi na kufuatilia hadi alipokutwa ndani ya gari la abiria liendalo runzewe.

Mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa katika hospital ya wilaya ya kahama, na mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi hadi uchunguzi utakapo kamilika. 
 Kisima alichotupwa mtoto huyo
Majirani wakiwa katika nyumba aliyokuwa anaishi mama wa mtoto huyo

TUMEAMIA HUKU