KHA! Staa wa Kerewa, Nurdin Bilal ‘Shetta’ juzikati
alijikuta katika wakati mgumu baada ya kumwagiwa uji wa moto na
Mbongo-Fleva mwenzake, Mwajuma Abdul ‘Queen Darleen’.
“Unajua leo ni siku ya kuzaliwa ya Shetta, ikiisha tu hii shughuli namuita nje na kummwagia maji yeye mwenyewe anajua sisi hatujui,” alisikika Ommy Dimpoz.
Baada ya tukio hilo ndipo Shetta alipotoka nje na kukutana na ishu hiyo ya kummwagia maji kisha Queen Darleen akamaliza mchezo kwa kummwagia uji.