Mtoto
Fabiani Masumbuko(4) mkazi wa tarafa ya Butundwe wilayani Geita
anadaiwa kunyanyaswa kwa kuunguzwa mikono yake na shangazi yake kwa kile
kinachodaiwa kuwa mtoto huyo alichukua kiazi kitamu bila ridhaa yake
na kukichoma kwenye moto ili baadaye akile kutokana na njaa aliyokuwa
nayo.
Tukio hilo limetokea tarehe 4 mwezi huu ambapo hadi sasa hivi shangazi wa mtoto huyo hajafahamika alipo mara moja baada ya kutenda unyama huo na kutoroka huku wasamaria wema waliomkuta mtoto huyo walimchukua na kumpeleka hospitali.
Kaimu
mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Geita George Rweyemela
amesema kuwa wamempokea mtoto huyo tarehe 5 kutoka kwa wasamaria wema
waliomleta lakini baada ya kumkabidhi waliondoka bila kuaga na na
kuwalazimu kuendelea kumtunza kwa uangalizi wa hospitali na kumhudumia
maana hawajui hata ndugu yake na wala hajajitokeza hadi sasa hivi''
Aliongeza kuwa kutokana na hari aliyokuwa nayo mikono ilikuwa imeunguzwa na sehemu za makalio tuliweza kumpima na kubaini kuwa ana ukosefu wa lishe kutokana na kukosa chakula kwa muda mrefu hivyowanaendelea kumpa matibabu.
Mwandishi aliyefika katika hospitali hiyo alimkuta mtoto huyo akifanya mazoezi ikiwa ni dalili za kuwa ameshaanza kupata unafuu huku akiongea kwa shida kutokana na maumivu aliyonayo.

Kamanda
wa Polisi mkoani hapa Joseph Konyo alithibitisha kupata taarifa za
mtoto huyo lakini uchunguzi wa kumtafuta mtuhumiwa bado unaendelea ili
ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.