Msanii Blandina Chagula 'Johari' baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la baba yake mdogo Mzee Clement Chagula.
Baadhi ya mastaa wa Bongo Muvi walioshiriki mazishi hayo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani Kikwete akiteta jambo na wasanii Steve Nyerere (kulia) na Mrisho Mpoto 'Mjomba'.
Mastaa wa Bongo Muvi wakiwa na Johari.
Kaburi la baba mdogo wa Johari, Mzee Clement Kiyenze Chagula.
STAA wa Bongo Muvi, Blandina Chagula 'Johari' amefiwa na baba yake
mdogo Mzee Clement Kiyenze Chagula aliyezikwa leo. Marehemu Chagula
amefariki akiwa na miaka 63. Mazishi hayo yalihudhuriwa na mastaa kibao
wa filamu nchini akiwemo Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani
Kikwete.