Miongoni mwa vitu vilivyokuwa vikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa bongo fleva wiki hii ni pamoja na kusikia kauli ya Alikiba kuhusu chanzo cha beef kati yake na msanii mwenzake Diamond Platnumz.
Kupitia
kipindi cha Sporah kilichoruka July 22 Clouds TV, Alikiba amefunguka
mambo mengi ikiwemo jinsi walivyofahamiana kwa mara ya kwanza, chanzo
cha beef yao na wakoje hivi sasa.
Kabla hujafahamu undani wa alichokizungumza, hizi ni facts chache alizozitoa Alikiba katika Interview hiyo.
1.Alikiba ndiye alimpa ruhusa Bob Junior amrekodie Diamond nyimbo zilizomtoa kama ‘Kamwambie’ katika studio yao ya Sharobaro!
2.Alikiba alishirikishwa katika wimbo wa Diamond ‘Lala Salama’!
3. Alikiba ni shabiki wa nyimbo za Diamond hadi sasa!
4. Diamond aliomba ashirikishwe katika hit ya Alikiba ‘Single Boy’!
5. Alikiba ana watoto watatu, lakini hana uhusiano tena na mama zao
Asilimia kubwa ya kipindi ilihusu uhusiano wa Alikiba na Diamond, na hii ni sehemu ya maelezo ya Kiba.
Alikiba
aliizungumzia sababu iliyozaa beef kati yake na Diamond, swali la
Sporah lilikuwa kama Alikiba ana namba ya simu ya Diamond:
“Nilikuwa
nayo kipindi Fulani, nilipohisi amenikosea nikaona sina ulazima…kuna
kipindi alinikosea kwasababu nilisikia amesema kwamba tulirekodi wote
ile nyimbo ya ‘Single Boy’, na si kweli. Halafu anasema mimi ndio
nilimfuta…
kwa
kunikosea kwa Diamond nilihakikisha kutokana na mimi mwenyewe ndo
nilifanya nyimbo yake ‘Lala Salama’ iko kwenye album yake, akanifuta
nikahisi amenikosea sana nilichoimba mimi akawa ameimba yeye,
alichonituma nifanye nimefanya kwa mapenzi yote, na mimi namsupport kila
msanii wa Tanzania anayefanya vizuri anayeimba vizuri, sikatai anaimba
vizuri sijui ukisema ame copy am proud, mi sijamaind wala nini lakini
usiseme kwa watu ukadanganya ukaonekana mi sifai, siko hivyo mimi.”
Aliendelea,
“Watu
wengine ambao hawaelewi vizuri wanaweza wakamwamini Diamond, kila mtu
ana mapenzi yake labda kuna wengine wanampenda Diamond wengine
wanampenda Alikiba. wanaweza wakawa wengine wanampenda Diamond wakaamini
mimi nimemfuta Diamond kwenye nyimbo ya ‘Single boy’ lakini mimi wala,
shahidi producer Manecky ndo alitengeneza ile nyimbo. Sikuwahi kwenda na
Diamond kwenye studio na sikuwahi kufikiria kufanya nyimbo nae.
Ila
alinipigia simu baada ya ile nyimbo kuleak, imevuja Single boy, tayari
nimeshafanya na Jaydee, akaisikia kwenye simu Ali kuna nyimbo nimeisikia
unaonaje ile tukifanya ile itakuwa safi sana afu akanipa mpaka idea ya
video na nini, nikamwambia sawa inawezekana lakini mimi nadhani
itapendeza zaidi tukifanya nyimbo nyingine mimi na wewe,kwasababu hii
tukifanya mimi na wewe haita make sense inapendeza ikiwa single boy
single girl, hicho ndo kitu nilimjibu.
Akaniambia
poa lakini we fikiria hiyo, nikamwambia okay lakini hata kama
nikifikiria mi sioni jibu hapo, jibu ni hilo hilo. Hicho ndo kitu
ambacho nilimjibu Diamond. Baada ya kama wiki moja nikaja kusikia kwenye
mablog, mpaka nikapigiwa simu kwamba mimi nimemfuta kwenye ile nyimbo
wakati yeye ndio aliyenifuta katika nyimbo yake, shahidi producer wangu
mimi KGT anaitwa ambaye nimetoka naye muda mrefu sana..nyimbo zangu zote
alikuwa akiproduce yeye”.
Kuhusu nani aliyemuita mwenzake kwaajili ya wimbo ambao Alikiba anadai Diamond alimfuta (Lala Salama)
“Hakuna
aliyemuita mwenzake, ila mimi pale studio ambayo alikwenda kurekodi
Diamond ni studio ya kwangu mimi ambayo ilikuwa imenitoa pale G-Records
na watu wote wanajua nimetokea pale. ..Nakwenda kutembea kama nyumbani ,
kuwatembelea studio kumtembelea producer wangu, nikamkuta Diamond nae
studio anarecord. Kuingia pale ndani ya studio nikakuta amesha record
kabisa…akaniambia hebu sikiliza hii, nikasikiliza nikamwambia umeimba
vizuri sana…nikajaribu kumwambia ungeimba hivi na hivi na hivi ingekuwa
vizuri sana ila niliheshimu mamuzi yake kwasababu kila mtu na style
yake, nikawa nataka kuondoka akaniita, akaniambia nakuomba uingize zile
sauti zako za juu, kila mtu anajua ukisema hivyo, kuna sauti zangu flani
hizo silaha zangu naweza kusema wengi wanapenda.
Nikamwambia
nikiingiza vile nitaharibu mi nahisi umeimba vizuri sana, akaniambia
imba bwana, atleast chochote kile, ndio nikaimba sasa mimi pale baada ya
kufanyaje, nimeona aibu kumkatalia mbele ya producer wangu. Ni Kwa
mapenzi yote nilifanya, nikamfanyia vizuri, kweli nilikwenda na feeling
nzuri sana kwasababu nyimbo ilikuwa ndio style yangu vile vile.
Lakini
sasa, kwasababu hata producer wangu hakuniambia nikaja kuisikia nyimbo
imetoka ameingiza yeye vile nilivyokuwa nikiimba mimi yaani njia
nilizokuwa nimepita akaingiza yeye, kwahiyo nikahisi kama amenifanya
mtoto wakati mimi ni mkubwa wake na anajua hilo”.
Baada ya Alikiba kugundua hilo alichukua hatua gani za kumuuliza Diamond au producer?
“Niligundua
kabisa producer wangu kunipigia simu mimi ilikuwa sio sawa kwasababu
ile nyimbo sio yake halafu nilimpa tu uhuru wa kufanya kazi na kila
msanii na nilijisikia vizuri Diamond amekuja mpaka pale studio kwetu
kufanya kazi ..
Mi
nilichukua simu yangu nikampigia Diamond, alichonijibu akasema yeye
mwenyewe hajui , basi mi nikaachana na haya mambo, from then nikaona
hamna tatizo lakini kwa kujua yeye alinifuta katika nyimbo yake”.
Alikiba na Diamond walivyofahamiana:
“Unajua
mimi Diamond nimemjua muda mrefu sana, mimi ndio nimemrelease pale
akafanya nyimbo Sharobaro wakati mimi niko kwenye tour America, nilikuwa
pale kama president, vice wangu alikuwa Bob Junior ambaye ndio producer
pale, akanipigia simu kwasababu hakuwa na maamuzi ya kumruhusu arekodi,
bana kuna msanii anaitwa Diamond anaimba vizuri tu, nikamwambia kama
anaimba vizuri mrekodie”.
Alikaba amekiri kuwa ni shabiki wa nyimbo za Diamond lakini si shabiki wake:
“Mimi
sijutii, vile vile am happy kwa yeye kufanikiwa kufanya kazi nzuri,
amerepresent nchi yetu anajitahidi kwasababu honestly naweza kusema
ukweli mimi pia sometimes nakuwa shabiki wa music..mimi sio shabiki wa
Diamond. Unapoongelea shabiki unaweza kushabikia nyimbo basi, kuna
nyimbo ambazo amenifurahisha Diamond ameimba nikasema yes amefanya
vizuri, lakini sio kwamba namshabikia yeye, mi napenda music, sikufichi
mi naskiliza music ya kila msanii anayeimba vizuri, siwakubali wasanii
napenda kazi zao”.
Kuhusu alivyojipanga kurudi kwenye game na kukabiliana na Diamond ambaye kwa sasa ndie msanii aliye juu zaidi:
“Kizuri kikikosekana kibaya pia kinaonekana kizuri…!!”
Sporah alimuuliza kuwa haoni kwa kipindi alichokaa kimya Diamond ndio kama amechukua nafasi yake kwenye muziki:
“Hakuna
mtu aliyechukua nafasi yangu, labda kama ni kiti ambacho nilikuwa
nimekaa kinavumbi na nachotakiwa ni kukipangusa tu na kukaa tena, lakini
labda yeye yuko siti nyingine ila the back seat. Formula tofauti najua
sasa hivi wanahitaji nini sababu muda ambao nimepumzika nilikuwa kama
mshabiki wa muziki…lakini sikuweza kupata muziki ule kama tulikuwa
tukisikia zamani Latifah…Violet ambao ule kama wimbo wa taifa. Na
nimeona wanamiss kwasababu mafans wangu kwa upendo wao kwakweli
nawashukuru sana kwa mapenzi ambayo wamenionesha uvumilivu na
kunikumbusha Ali njoo we need you…and kwa respect ambayo nimewapa
nawaambia Alikiba himself anakuja tena very soon, now new material, new
look, na next level kila kitu”.
Ujumbe wa Alikiba kwa mashabiki wake:
“Asabteni
tena na tena (mashabiki) malalamiko yenu nimepata sana, samahani najua
nimewa letdown, kama mlivyoona wengine wamepata chance ya kushine na
wakatuwakilisha kwasbabu tu Alikiba aliwaachia nafasi hiyo…narudi tena
very soon so get ready for this na mnipokee vizuri.”
Siku
mbili zijazo Alikiba ataachia wimbo wake mpya unaoitwa ‘Mwana Dar es
salaam’.Stay tuned! ‘mwenyekiti’ chake ndo kaishakipangusa vumbi so
wengine waende chumbani wakalale? (na watuache tulale) LOL!