Walezi
wa kwaya ya Mtakatifu Aloyce Gonzaga Jimbo Kuu la Dar es Salaam,
Francis Mihayo (kushoto) na Sylvester Tyienyi wakiwa na kichanga
kilichoopolewa chooni mkoani Tanga ambacho kimetimiza mwezi mmoja sasa.

Mlezi
wa kwaya ya Kanisa Katoliki la Mtakatifu Aloyce Gonzaga Parokia ya
Mtakatifu Yohana Mbatizaji Luhanga Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Francis
Mihayo, akiwakabidhi watoto wa kituo cha kulelea Watoto Yatima cha Casa
Della Diaia (Nyuma ya Furaha) cha Bombo Tanga, msaada wa vyakula na vitu
mbalimbali walipotembelea kituo hicho.
Francis
Mihayo akimkabidhi mlezi wa watoto wa kituo cha Casa Della Dioia
(Nyumba ya Furaha), Sister Consolata cha Bombo Tanga msaada wa vyakula
na vitu mbalimbali.
Francis
Mihayo akiwa amembeba mmoja wa watoto waishio katika mazingira magumu
wa kituo cha Casa Della Dioia (Nyumba ya Furaha) wengine wakiwa
wamemzunguka.
KICHANGA kilichoopolewa kutoka chooni maeneo ya Pongwe mkoani Tanga kimetimiza mwezi mmoja sasa.
Kichanga hicho kiliopolewa na wasamalia wema na baadaye kupelekwa
katika kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Casa Della Diaia (Nyuma ya
Furaha) na sasa kimetimiza mwezi mmoja tangu kikabidhiwe katika kituo
hicho na hali yake ya kiafya inaendelea vizuri.
Wanakwaya wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Aloyce Gonzaga, Parokia ya
Mtakatifu Yohana Mbatizaji Luhanga Jimbo Kuu la Dar es Salaam
walibahatika kutembelea kituo hicho na kutoa msaada wa vyakula na vitu
mbalimbali wakiwa katika ziara ya kutembelea parokia tarajiwa ya
Mtakatifu Yohana Mbatizaji ya Jimbo Katoliki la Chumbageni mkoani Tanga.
Kituo hicho kina jumla ya watoto 47, mtoto mkubwa akiwa na miaka 22 na mdogo ana mwezi mmoja.