Featured Posts

Friday, July 25, 2014

HILI NDIYO PENZI TAMU ZAIDI..JARIBU MWENYEWE UTAKUBALI

PENZI ni tamu sana kila mtu anatambua hilo,
na kukoswa pendo ni uchungu sana katika
maisha ya binadamu. Pamoja na hayo
yawezekana wewe
unayesoma blogu hii na wewe unampango
wa kumuacha mpenzi wako, kutokana na
sababu mbalimbali lakini yote hayo ni sawa 
na kupotea ndugu yangu.
Nakuomba sana usimuache mke wako
kwani daima ulishamutamkia kuwa
unampenda na hutamuacha kamwe katika
maisha yako! Kumbuka baada ya kumuacha
mrembo bibie utapata nini au utafaidika na
nini?
Zaidi ya kuanza kujuta na kuumia roho
yako? Wapo wanaume wengi wanaoachana
na wake zao matokeo yake wanaanza
kujutia kitendo hicho. Namkumbuka baba
mmoja tajiri mkubwa katika jiji hili la Dar
aliwahi kuja katika ofisi zetu za ushari ili
kuomba ushari wa doa yake Baada ya mke
wake kuchoshwa na baba huyo na kuamua
kurudi kwao Mwanza.
Sasa baada ya kuachwa baba huyo alianza
kuumia zaidi na kuwa anashinda nyumbani
badala ya kwenda kazini, jambo ambalo
lilimpelekea kuja ofini kwetu kuomba
ushauri wa kufanya ili mke wake arudi. Nasi
tulimpatia ushauri na tukamuita mke wake
naye tukamupa ushauri wa umuhimu wa
mke na mume katika ndoa, jambo ambalo
liliwaunganisha na mpaka sasa wanaishi
kwa amani na upendo wa ajabu.
Sasa ndugu yangu kumbuka kuwa
mwanamke ni muhimu sana katika maisha
yako, mwanaume ameumbwa kwa ajili ya
mwanamke na mwanamke kwa ajili ya
mwanaume sasa kunahaja gani ya
kumtukana mke wako ambaye ni mzuri?
Kunahaja gani ya kumfukuza mke wako
anaye kupa penzi la dhati?
Na kunahaja gani ya kuwa na msongo wa
wawazo kisa mke wako mwenye penzi
tamu kaondoka?
Sasa mwambie mke wako nakupenda sana
mke wangu na sitakuacha kamweeeee

TUMEAMIA HUKU