NAAM
kama ilivyo ada yetu, tumekutana tena kwenye kona yangu mimi shangingi
mstaafu mwingine fotokopi, nasikia kuna watu wanajiita mashangingi
wastaafu sifa yao kubwa kunywa pombe za watu na kuambulia kipigo mikovu
kama kibaka mzoefu.
Siku
zote tutashindana lakini mimi nitabakia namba moja, najua ujuayo na
usiyojua, kaa chini mwali nikufunde ulikimbia unyago hujui mizungu
inaokotwaje. Ndiyo maana nikasema mtashindana lakini hamtashinda namba
moja nitabakia mwenyewe.
Wapo
wanaotaka eti tukutane hadharani tuoneshane nani zaidi, bado
nakuelezeni msipoteze muda wenu kunijadili moja mpaka kumi nimekamata
mie sijui ninyi wenzangu mmeshika namba ngapi hammo hata kwenye kumi
bora.
Hebu
nipishe niwape raha au unataka umaarufu kupitia jina langu, sikukatazi
lakini kimoyomoyo unajua kabisa anti Nasra namba moja yake mpaka kumi
ila kuanzia kumi na moja kanyaganeni huko siwaingilii.
Hebu tuzungumze kilichotutoa majumbani kwetu na kununua gazeti kisha kuisoma kona hii.
Leo
nataka kuzungumza na mijanamume yenye kukimbilia kwa waganga kuongeza
ukubwa wa nyeti. Jamani nakuulizeni ninyi waganga wa kienyeji mnaoongeza
ukubwa wa bakora mnajua ukubwa wa chungu anachokwenda kuingiza mwiko
wake?
Unajisikia
raha gani unapoingiza mwiko kwenye chungu, mwenzio anauma meno kwa
maumivu nani alikuambia raha upate wewe peke yako. Basi leo nataka
kuwaelezea kitu kimoja hasa ninyi mnaojiona bakora zenu fupi.
Usikimbilie
kwa mganga kuongeza ukubwa, nani aliyekuambia ukubwa wa mkono ukoleza
utamu wa ngoma. Au udogo wa mkono hupunguza utamu wa ngoma?
Hebu
nisikilize tena nisikilize kwa makini kutomfurahisha mpenzio si udogo
wa mwiko bali kujua kuutumia, unakimbilia kuongeza ukubwa wa nanihino
ili umfurahishe mkeo au umkomoe?
Siku
zote vita ni mbinu si manguvu mengi, vilevile utamu wa mahaba uwe
mtundu wa kujua nikae engo gani mpenzio anapokuwa amekaa mkao fulani.
Wengi najua hamjui matumizi ya mitindo ya mapenzi (Style) maana ya
mitindo ya mapenzi ni kutokana na maumbile ya mwanaume.
Kama
mafupi mpenzio unatakiwa umuweke mtindo gani kama marefu vile vile
mpenzio unatakiwa umuweke mtindo gani.Ukishajua matumizi ya staili za
mapenzi hutasumbuka kukimbilia kwa waganga, hivi nani aliyekuambia mpaka
ufike chini ya mchanga ndipo mpenzio apate raha, jamani raha
zinapatikana hata mwanzo mwa kisima kwa kujua kuteka maji kwa kata.
Huchoti maji mengi jaza kidogo… kidogo… kidogo… kidogo, hebu kajaribu umsikie mpenzio atakupa salamu gani.
Pia nataka kuwaeleza wote wanaokimbilia kuongeza ukubwa wa bakora zao, mnajua madhara yake?
Basi
nataka kukueleza maumbile yaliyo bora ni yale uliyoumbiwa na Mungu,
ukiyaongeza baada ya muda huishiwa nguvu na kujikuta kwenye tatizo
lingine la kutafuta nguvu za kiume.
Waulize
waliyoongeza ukubwa sasa hivi wanajuta ngoma ikilala hainyanyuki tena
wamebakia kula kwa macho mikono kupapasa bila kufaidi. Bakora zao
zimebakia kama magobore ya mbao hayana kazi bora wayakate wawashie moto
wa kuchemshia maji.
Hivi
jamani kucha zinazokuna kwa raha fupi au ndefu, siku zote kucha fupi
zina raha zake, ukiwa na kucha ndefu huwezi kumkuna mtu zaidi ya
kumuumiza na kumsababishia vidonda.
Nina imani nimesomeka, basi ndiyo mimi Anti Nasra Shangingi Mstaafu.
Milioni 392 Zajenga Barabara HEWA Dar es Salaam
-
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob amebaini matumizi ya Sh392
milioni zilizoandikwa kwenye taarifa ya manispaa hiyo kuwa zimetumika kwa
ajili y...