Love is blind lakini wanaopenda wana macho. Hapa inajidhihirisha kwa Chuchu hans, baada ya kuzunguka sana mwisho wa siku kufika alipotaka. Mwanadada huyo alikuwa Miss Tanga 2010 na kuingia bongo movie yuko ndani ya mapenzi mazito sana na legend wa bongo movie Raymond Kigosi a.k.a Ray , ceo wa RJ company.
Katika kuonyesha how deep her love kwa kijana huyo Chuchu aliamua kujichora tatoo yenye jina na Star huyo na kwa sasa Ray ameshahama kwao na kuhamia sehemu nyingine kuishi na binti huyo wa kitanga mwenye muonekano wa point five yani chotara flani na kwa sasa wawili hao wanaishi pamoja. So kama kuna anaesubiri waachane leo au kesho basi wawili hawa bado wapo sana na hata ndoa haitakuwa mbali sana kwani vibe ilipombana mdada huyo alijikanjaga na kuropoka kwamba target yao ni kuoana ila hajajua itakuwa lini lakini lazima ndoa itakuwepo , basi tuwatakie kila la kheri wawili hawa…