Hadi hii leo Divas maarufu waliowahi kufunguka kiundani kuhusu kutoka na mwanamuziki huyu, na kwa nyakati tofauti kila mmoja wao alijaribu kufunguka kuhusu experience zao, pindi walipokuwa wanatoka na mkali wa bongo fleva nchini hivi sasa Mr.Dangote aka Diamond Platnumz, ambaye amerudiana na kuendelea kudumu katika penzi lake la zamani na la siku zote kwa Diva Wema Sepetu..basi haya ndo machache waliowahi kutoa ya moyoni.
DVJ Penny
“Kama uhusiano wowote ulivyo, kuna mwanzo na mwisho na watu wanaachana kwa sababu nyingi. Nilihisi kwamba nahitaji kumpa nafasi, wote ni vijana na wakati mwingine tunahitaji nafasi kugundua vitu vipya, kuona kipi hasa unachokihitaji kwenye maisha. Unajua ukimruhusu ndege afanye vitu mbalimbali then atajua kama ‘mti huu ndio unanifaa, mti huu haunifai. Hivyo nilihisi kwamba wote tulihitaji hicho, tulihitaji ‘space’ hivyo nikampa nafasi na mimi nakuchukua nafasi. Huwa nawaambia watu kuwa vyovyote ilivyo, yeyote atakayekuwa naye, nipo pembeni yake nikimshangilia kwasababu ni kweli (Diamond) ni mtu mzuri ndani. Achana na watu wanavyomuona chizi chizi, sahau msanii unayemjua, ana roho nzuri na anajua anachokitaka. Ni ngumu kuacha iende.. kama ni rahisi kuacha iende basi hujampenda huyo mtu.”
Jokate Mwegelo
“Mahusiano ya diamond yalikuwa very strange, I dont know yani..i think ilikuwa kazi lakini I guess it was a time I guess I was frustrated,sielewi yani ilitokea tokea tu”
Jackline Wolper
“Ni kweli niliwahi kuwa na diamond,tulikuwa na mahusiano lakini pia alikuwa ni mshirika wa biashara,yeye alikuwa hawezi kulala bila kuniona,lakini tulidumu kama mwezi mmoja hivi, tukaishia kuwa marafiki tu.”