TUNAMALIZIA makala haya ya Sabrina Rupia ‘Cathy’ tuliyoyaanza wiki tatu zilizopita, mwigizaji huyu alifunguka mambo mengi kuhusiana na maisha yake, bila shaka kupitia mfululizo wa makala haya, msomaji utakuwa umejifunza vitu vingi kutokana na hatua ambazo amepitia maishani na leo hapa anafunguka kuhusu anavyofurahia maisha ya ndoa kwa kuolewa na mume ambaye amemzidi umri
SHUKA NAYO…
SHUKA NAYO…
Mwandishi: Kwa nini ulipenda mumeo akuzidi umri?
Cathy: Kwanza nilipenda busara zake na namna anavyonilea kama mtu wake wa karibu, si mtu wa mbwembwe kama walivyo wengine, namfurahia kwa sababu tunafanya maisha ya kweli, lakini nilitaka kupata mwanaume mwenye huruma ambaye hatoniumiza kama wafanyavyo vijana kwa sababu ya maisha ambayo nimeyapitia ya kuwa mpweke baada ya kufiwa na baba yangu.

Mwandishi: Una watoto wangapi kwa sasa?
Cathy: Sipendi kutaja watoto ila fahamu ni mama wa familia.
Mwandishi: Je ndoa uliyonayo ni ya ngapi kwako?
Cathy: (Anatahamaki kidogo) We! Ndoa ya ngapi? Hii niliyonayo ni ya kwanza na mwisho!
Mwandishi: Vipi kuhusu mameneja wako katika kazi za uigizaji hawakusumbui suala la kukusimamia bila kuwapa tunda la mumeo.

Cathy: Hapana najitambua lakini pia najivunia kuwa mme wangu ndiye meneja wangu kwa hiyo tunda ni halali yale kabisa.
Mwandishi: Ni kweli Bongo Muvi hamko tayari kuwatoa wasanii wachanga?
Cathy: Kwa kifupi hela zinaenda kwa wenye hela, hata mimi naweza kulalamika lakini nikipata nitachukua waliopata wenzangu na kuwaongezea na wale wapambane kutoka.
Mwandishi: Kwa nini msibebane?

Cathy: Ninachojua cha msingi ni kufaiti unavyojua mwenyewe lakini usikae kwa kumsubiri flani atoke ili akupe kiki hakuna mtu wa kukufanyia hivyo.
Mwandishi: Duuh! Kwa hiyo kila msanii anatakiwa kujibeba kivyake?
Cathy: Nafasi huwezi kupewa cha msingi ni kupigana na kutafuta upenyo wa kutoka iwe kwenye muvi au nje ya sanaa.

Mwandishi: Mpaka sasa una filamu ngapi?
Cathy: Kama nne au tano, kuna DNA, Wheel Chair nilifanya na Cloud, Saa Nne, Kaburi na Simu ya Mkononi ambazo hazijatoka.
Mwandishi: Nini ushauri wako?

Cathy: Watu wasibweteka hasa kina dada watumie nguvu zao kufanya kazi lakini pia wasanii wachanga wafaiti wenyewe wasisubiri kuolewa, kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake.
Mwandishi: Unazungumzije suala la ajira kwa vijana?

Cathy: Wanyanyuke waache uzembe kwani hata kilema anatamani japo anyanyuke kwa dakika kadhaa ili atembee, asiye na mikono anatamani angekua nayo ili imsaidie japo kulima sembuse wewe uliyekamilika unashindwa kujisaidia mpaka usubiri kutolewa!