Wanajeshi wa Boko Haram wanaofanya mashambulizi na kuua raia wasio na hatia huko Nigeria wamedaiwa kuanza kukimbia msitu baada ya nyoka wenye sumu kali na nyuki kuwashambulia.
Habari hizi zilielezwa na mtuhumiwa mmoja aliyekamatwa na kuthibitisha kuwa ni mmoja wa member wa kundi la Boko Haram na alieleza kuwa hivi sasa kundi hilo limelazimika kuhama msitu na linaelekea maeneo ya mpaka wa Nigeria na Cameroon baada ya wanajeshi wake wa ngazi za juu kushambuliwa na nyoka na kupoteza maisha.
Jeshi la Nigeria limeshafanya juhudi za kuwaondoa msituni lakini imeshindikana na hadi sasa kundi hilo linawashikilia wasichana zaidi ya 260 na bado linaendelea kushambulia Nigeria kwa mabomu ya kutegwa.