Featured Posts

Wednesday, June 25, 2014

BAADA YA UVUMI JUU YA KIFO CHA WAZIRI WA ELIMU NDG. SHUKURU KAWAMBWA HILI NDILO TAMKO RASMI JUU YA UVUMI HUO

Ndg Watanzania,WanaBagamoyo na wapenda maendeleo, kwa niaba ya CCM-Bagamoyo na Ofisi ya Mbunge-Jimbo la Bagamoyo napenda kuleta kwenu Masikitiko yetu kwa niaba ya Chama na Familia ya Mheshimiwa Mbunge Shukuru Jumanne Kawambwa kutokana na Usumbufu ambao umesababishwa na habari zinazoenezwa Mitandaoni kwamba Mheshimiwa Kawambwa amekumbwa na Umauti akiwa njiani anaelekea Mwanza.

UKWELI
Mheshimiwa Shukuru Jumanne Kawambwa yupo Nchini Canada Akitimiza majukumu yake. Hivyo Watanzania na wana Bagamoyo mnaombwa radhi kwa usumbufu uliotokea na kwamba Mheshimiwa Mbunge yuko na Afya njema na utekelezaji wa Majukumu unaendelea kama kawaida.


Ndg.Ridhiwani Kikwete (Mnec)
Mbunge -Chalinze 

TUMEAMIA HUKU