Staa wa kike anayefanya vizuri katika tasnia ya fillamu Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ amefunguka na kudai kuwa hajawahi kula hela ya mume wa mtu na kama watu wanamhisi hivyo basi watakuwa wanakosea sana…..
Batuli alitoa kauli hiyo ili kuwathibitishia mashabiki wake juu ya kauli mbovu za watu kuwa urembo wake unategemea mtaji wa mwili wake ambapo amewajibu kwa kusema kuwa urembo na uzuri wake unatokana na matunda ya kazi yake ya sanaa na kimsingi anautumia huko kwa kuwa haoni faida ya kula hela ya mwanaume kwani hajaifanyia kazi…..
“Amini kuwa naendesha maisha yangu kwa misingi ya kazi zangu, inawezekana wapo wanawake wanaoishi mjini kwa kutegemea mtaji wa miili yao na si sanaa.
” Kwa upande wangu hata Mungu ananiona kuwa kile ninachokipata kupitia sanaa ndicho ninachokitumia kwenye matumizi yangu,” alisema Batuli