Featured Posts

Wednesday, June 25, 2014

BATULI AFUNGUKA KUHUSU KULA PESA ZA WAUME ZA WATU

Staa  wa  kike  anayefanya  vizuri  katika  tasnia  ya  fillamu Yobnesh Yusuph ‘Batuli’   amefunguka  na  kudai  kuwa  hajawahi  kula  hela  ya  mume  wa  mtu  na  kama  watu  wanamhisi  hivyo  basi  watakuwa  wanakosea  sana…..
 
Batuli  alitoa  kauli  hiyo  ili  kuwathibitishia  mashabiki  wake  juu  ya  kauli  mbovu  za  watu  kuwa  urembo  wake  unategemea  mtaji  wa  mwili  wake  ambapo  amewajibu  kwa  kusema  kuwa    urembo  na  uzuri  wake  unatokana  na  matunda  ya  kazi  yake  ya  sanaa  na  kimsingi  anautumia  huko   kwa  kuwa  haoni  faida  ya  kula  hela  ya  mwanaume  kwani  hajaifanyia  kazi…..
Mwanadafada mkali wa Bongo Movies, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’.
Mwanadafada mkali wa Bongo Movies, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’.
 
“Amini  kuwa  naendesha  maisha  yangu  kwa  misingi  ya  kazi  zangu, inawezekana  wapo  wanawake  wanaoishi mjini  kwa  kutegemea  mtaji  wa  miili  yao  na  si  sanaa.
 
” Kwa  upande  wangu  hata  Mungu  ananiona  kuwa  kile  ninachokipata  kupitia  sanaa  ndicho  ninachokitumia  kwenye  matumizi  yangu,” alisema  Batuli

TUMEAMIA HUKU