
Basi la Amani Express likitokea Kigoma kuelekea Dar es salaam limepata ajali usiku wa kuamkia leo maeneo ya Salanda mkoani Tabora, ambapo mtoto wa miaka mitatu amepoteza maisha na abiria kadhaa wamepata majeraha.
Mashuhuda wanahisi kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi. Pichani abiria wakitafuta vitu vyao


Baadhi ya abiria walionusurika katika ajali hiyo wakisubiri msaada wa usafiri

Basi la Amani likiwa limepinduka