mitandao
ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari Bongo kwamba msanii wa Bongo
Fleva, David Genzi ‘Young Dee’ na nyota wa filamu,Elizabeth michael
lulu wamebambwa na polisi wa diria wakivunjaamri ya sita ndani ya gari
aina ya Hyundai, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, tukio lililojaa utata
mkubwa.
Kwa
mujibu wa habari hizo, wawili hao walinaswa wakifanya uchafu huo na
askari waliokuwa doria lakini wakawavuta chobingo na baada ya muda,
wakawaachia na kutokomea kusikojulikana.
Ili
kupata ukweli wa tukio hilo la aibu, paparazi wetu alianza kwa kumvutia
waya Young Dee na kumsomea mashtaka yake ambapo alifunguka kuwa ni
kweli amezisikia habari hizo lakini akakana kwamba ishu hiyo siyo ya
kweli bali imezushwa na kundi la watu wenye lengo la kumharibia jina
lake mbele ya jamii.
“Siyo
kweli kabisa, isitoshe nina kama mwezi mzima sijaonana na huyo Lulu,
huku ni kutaka kuchafuliana majina tu,” alisema Young D.
Habari
zinadai kuwa licha ya Young Dee kukanusha kuwa hajaonana na Lulu kwa
muda mrefu, siku ya tukio walikuwa pamoja ingawa hawakutaka kuonekana na
mtu yeyote.
Kwa
upande wa Lulu alipotafutwa, alifunguka: “Kweli nimesikia ishu kama
hiyo ila kinachonishangaza na kunisikitisha ni kwamba siku hiyo ya tukio
inayotajwa mimi nilikuwa nyumbani na siku nzima sikutoka kwenda popote,
hata hiyo Mbezi iliyotajwa mimi siielewi kabisa, hata lile gari mimi
sina gari la aina hiyo wala sijawahi hata kulipanda gari hilo na huyo
Young Dee nina muda mrefu sana sijaonana naye,”
“Usiku
wa kuamkia leo nilimpigia mtangazaji mmoja ambaye aliirusha habari hiyo
redioni, nikataka kujua ameipata wapi habari hiyo? Akanijibu kwamba
amepata tetesi tu. Sasa kama ni tetesi kwa nini asichunguze kabla
hajanichafulia jina?”
“Pia
alisema kuna askari wa doria walitukamata, nikamtaka anipeleke hicho
kituo cha polisi tulikopelekwa ili tuthibitishe kama ni kweli maana ishu
hii inanichafua mimi na familia yangu, akashindwa kufanya hivyo.
“Yaani
naomba ieleweke kuwa sijafumaniwa na siwezi kufumaniwa na mtu kama
Young Dee maana kwanza hata sijawahi kukutana naye hivi karibuni,
sipendi kuchafuliwa na haya yote namuachia Mungu atawajibu wote
wanaonizushia,” alisema
Milioni 392 Zajenga Barabara HEWA Dar es Salaam
-
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob amebaini matumizi ya Sh392
milioni zilizoandikwa kwenye taarifa ya manispaa hiyo kuwa zimetumika kwa
ajili y...