Featured Posts

Thursday, July 31, 2014

RAY NA CHIKI WAZIDI KUTIFUANA, SOMA HAPA UNDANI WA BIFU LAO HAPA

BAADA ya kuibuka sintofahamu kati ya waigizaji wa Bongo Movies, Salum Mchoma ‘Chiki’ na Vincent Kigosi ‘Ray’, Chiki ameibuka na kuzungumzia ishu hiyo.

Staa katika tasnia ya filamu Bongo Vincent Kigosi ‘Ray’,
Akipiga stori mbili tatu na paparazi wetu, Chiki alisema kuwa yeye na Ray hawakuwahi kuwa na bifu kama inavyozungumzwa kwenye mitandao ya kijamii isipokuwa walipishana kauli kidogo katika bethidei ya muigizaji Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ iliyofanyika katika Hoteli ya Lamada, Ilala jijini Dar lakini waliyamaliza.
“Sina bifu na Ray tuko poa, pale Lamada tulipishana maneno kidogo tu ila kwa sasa stori kama kawa hatuna bifu la aina yoyote,” alisema Chiki.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo Salum Mchoma ‘Chiki’.
Kwenye bethidei hiyo, ilidaiwa kuwa Chiki aliyekuwa MC wa shughuli hiyo alimpa maneno ya ‘madongo’ kumsisitiza atoe mkwanja ‘fedha’ nyingi kama zawadi kwa Dk. Cheni hali ambayo ilimuudhi Ray.
Imeandikwa na Maria Halimoja na Rhoda Josiah.

TUMEAMIA HUKU