Featured Posts

Thursday, July 31, 2014

TUNDA MAN YAMKUTA MAZITO

Memba wa Kundi la Tip Top Connection, Khalid Ramadhan ’Tunda Man’ amekutwa na mauzauza baada ya kupokea simu yenye namba zinazodaiwa kuwa za ajabu na kumsababishia atokwe damu puani, mdomoni na kupooza upande mmoja.

Memba wa Kundi la Tip Top Connection, Khalid Ramadhan ’Tunda Man’ akiwa katika Hospitali ya Palestina.
Chanzo makini kilicho karibu na msanii huyo ambacho kilikuwa ndani ya Hospitali ya Palestina ambako Tunda Man alilazwa, kimeeleza kuwa, tukio hilo lilitokea mwanzoni mwa wiki hii wakati staa huyo akifuturu.
“Alipigiwa na namba f’lani hivi ya ajabuajabu inayoishia na 39 kama mara 30 hivi, hakuipokea maana alishawahi kusikia juu ya namba za ajabu lakini baadaye akaamua kupokea ndipo ghafla akaanguka, akaanza kutokwa damu puani kisha kuzimia kabisa,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Tulimfikisha Hosptali ya Palestina na hali yake ilikuwa mbaya sana lakini kwa jitihada za madaktari na manesi wamemsaidia kwa sasa kidogo anaendelea vizuri.”
Khalid Ramadhan ’Tunda Man’.
Baada ya kupata taarifa hiyo, Ijumaa lilimtafuta Tunda Man ili kutaka kujua undani wa sakata hilo, alipopatikana alifunguka:
“Nakumbuka nilipokea simu yenye namba nisizozifahamu ambayo iliita sana nikajishtukia kuipokea lakini baadaye nikahisi ni kama namba za nje ya nchi labda ni dili la kwenda kufanya shoo, nilivyopokea tu sikuwa nasikia mtu akiongea zaidi ya kusikia mtu kama vile anapuliza kitu.
“Baada ya hapo nikajiona naishiwa nguvu, damu zikinitoka puani na mdomoni kisha nikajikuta nipo Hospitali ya Palestina,” alisema Tunda Man.

TUMEAMIA HUKU