WASANII wa Tanzania wenye mashabiki wengi Afrika Mashariki, Lady Jay Dee na Diamond Platinumz, wameitoa Tanzania Kimasomaso kwa kushinda tuzo moja moja katika tuzo za AFRIMA (African Muzik Magazine Awards 2014), zilizofanyika jana Dallas, Marekani.
Kwa mujibu wa mtandao wa African Music Magazine, Lady Jay Dee alishinda tuzo ya mwimbaji bora wa kike wa Afrika Mashariki na Diamond Platinumz alishinda tuzo ya Msanii bora wa kiume wa Afrika Mashariki.
Hata hivyo, kwa habari ambazo zimeenea Tanzania na kutajwa kuwa zilizotolewa na meneja wa Diamond zinaeleza kuwa Diamond ameshinda tuzo mbili ambayo nyingine ni wimbo bora wa kushirikiana.
Hali hiyo ilisababisha utata, kwa mashabiki wa mwanamuziki huyo Diamond Platnamu hali iliyopelekea mashabiki hao kuhisi kuwa msanii huyo amewadanganya mashabiki wake.
Lakini kwenye orodha halisi ya mtandao a AFRIMMA, tuzo ya wimbo bora wa kushirikiana imeenda kwa Mafikizolo feat Uhuru (Khona).
Kwa mujibu wa maelezo aliyoandika Diamond kwenye Instagram, inaonesha kama ameshinda tuzo zaidi ya moja.
“First of all napenda nimshkuru sana Mwenyez mungu, Mama, Family, My management, kipenzi changu, Media, bila kuwasahau nyinyi mashabiki zangu pendwa kwani sikuzote mmekuwa mkinisupport bega kwa bega kwenye shida na raha...Niwashkuru pia Wasanii wenzangu toka nje na ndani ya Tanzania kwani naamini changamoto tunazopeana ndio zimefanya hadi sasa mziki wetu ufikie hapa...hakika tunzo hizi si zangu bali ni za Muziki wa Bongo flavour... Mwisho kabisa nimshkuru Mh Rais Jakaya Mrisho kikwete kwa mchango wake wa kila siku katika sanaa yetu!... Mr President your Son Did it!!!!! #MdogMdogo.”