Mapema leo nilikupatia story kuhusiana na kijana matata Richard Mollel pesa chafu ambaye amejipiga risasi Arusha, sasa nimepata muendelezo wa matukio ya ajabu yaliyomtokea kijana huyo kabla ya kifo chake mpaka alipojiua.
Yaani ndio nimetokea hapo kwake kwani ni ajabu kabisa.
Alikuwa na girl friend wake kwenye gari kufika eneo la Mount Meru akagonga Hiace kwa nyuma gari ikabonyea lakini yeye na mpenziwe wakatoka wazima bint anadai baada ya dakika km 2 akahisi kizunguzungu akaanguka chini kuja
kushtuka anaona watu wengi na kijana naye kutoka hapo akatimka mpaka karibu na nyumbani kwake ndio kujipiga risasi na kufa.
Sasa binti anaulizwa mlikuwa na ugomvi anasema wala yeye mwenyewe anashangaa kilichomkuta keshatoka mzima kwenye ajali kukimbia na kwenda kujiua.
Ni kijana wa 86 yaani mdogo kabisa na ndio pesa imekubali na baba yake ni mgonjwa yuko hoi muda huo yenyewe alikuwa amepigiwa simu na dada zake aende kumuogesha maana ni mtoto pekee wa kiume na ndio alikuwa anaenda sasa hawajui ni kitu gani kilimkumba kuamua kujiua.